Idadi
kubwa ya watu linapokuja suala la pesa, wapo makini sana na tabia kama
kupanga mipango mizuri, kutumia pesa kwa busara na hata ikiwezekana
kubana matumizi ili kuhakikisha usalama wa pesa unakuwepo.
Lakini,
hata hivyo pamoja na wengi kijitahidi kufanya hivyo, bado zipo tabia
ambazo watu wanazo zinawaacha au zinasababisha wengi kuendelea kubaki
kwenye umaskini ingawa ukiangalia pia watu hao wana uwezo wa kupata pesa
kila wakati.
Kwa
hiyo hapa unaona tatizo la watu wengi sio kupata pesa, kama ni pesa
kweli wanazipata, ila shida inakuja kwa kukumbatia tabia hizo ambazo
zinawarudisha nyuma sana na matokeo yake kuwaacha katika dimbwi la
umaskini.
Leo
hapa katika makala haya, tunakuletea tabia mbaya ambazo kwa mtu yeyote
akiwa nazo ni lazima mtu huyo ataendelea kubaki kwenye umaskini. Hakuna
ujanja katika hili, kama una tabia hizi, nimesema utaendelea kubaki kuwa
maskini.
1 Weka kumbukumbu ya pesa zako.
Haijalishi
unakipato kikubwa au una kipato kidogo, kuandika matumizi yako ni jambo
la lazima ili uweze kufanikiwa. Kitendo cha kuwa na kumbukumbu na
matumizi yako si suala la kumwachia Bill Gates peke yake hata wewe
linakuhusu.
Huhitaji
kutumia pesa zako tu hovyo kwa sababu eti unazo, unachotakiwa kujua ni
wapi kila pesa yako inakwenda. Zoezi hili litakusadia sana kuwa makini
na pesa zako na kukuokolea pesa nyingi ambazo zingepotea bila sababu.
Hili
jambo liko wazi, hutaki kuweka kumbukumbu zako vizuri, utake usitake
huwezi kutoka kwenye umaskini hata ufanyeje. Kama unabisha wafatilie
watu wenye pesa nyingi sana, utaona hili wanalifanya sana maishani mwao.
2. Mhemko wa matumizi.
Tunaposema
mhemko wa matumizi ni kufanya matumizi ya pesa kwa kutawaliwa na hisia
zako. Hapa unakuwa unafanya matumizi kwa kuongozwa sana na hisia na
unakuja kushituka kile kipindi ambacho pesa zako zimekwisha.
Kwa
mfano, kwa sababu una pesa kila kitu kinachopita machoni mwako unataka
unanunue, zizikipita nguo unataka kununua, kikipita kitu hiki au kile
unataka kununua pia, huu ndio mhemko wa matumizi tunaouzungumzia hapa na
ni tabia mbaya ya kipesa..
Watu
matajiri wapo makini sana na matumizi yao, na hiki kitu hata wewe
unatakiwa kuwa nacho ili kutengeneza utajiri wako. Pia kama hutaki kuwa
makini na matumizi yako na kutawaliwa na mhemko, elewa utaendelea kubaki
maskini.
3. Kung’ang’ania njia moja ya kipato.
Kati
ya hatari kubwa sana ambazo watu wengi wanacheza nazo na inawaacha
kwenye umaskini ni kung’ang’ania kuendelea kuwa na njia moja ya
kuengeneza kipato. Utakuta mtu anapata pesa nyingi kweli lakini njia ya
kipato kimoja inamuangusha.
Najua
unawajua watu ambao walikuwa wakifanya kazi kubwa na zenye mishahara
mikubwa, lakini mara baada ya kuacha kazi unashangaa maisha yao yako
hovyo sana. Yote hiyo inasababishwa na kuwa na chanzo kimoja cha kipato.
Labda
tuseme hivi, utake usitake kama una njia moja ya kipato kuendelea
kubaki maskini kunakuhusu kwa asilimia mia moja. Pigana na hali yako kwa
kila namna uweze kutengeneza njia nyingne ya kutengeneza kipato, ndio
utatoka..
4. Kukosa uvumilivu.
Sikuzote
ili kupata pesa hakuji mara moja tu, ni zoezi ambalo linahitaji sana
uvumilivu na kuchapa kazi kwa juhudi zote. Wengi wanashindwa kujua hili
na kushindwa kuwekeza kwenye vitega uchumi ambavyo vingewapa pesa nyingi
kwa baadae.
Kama
unatabia za kutaka kupata pesa nyingi kwa chapu chapu na kushindwa kuwa
mvimilivu sahau jambo hili. Unatajiri una kawaida ya kujengwa hatua kwa
hatua hadi kufikia kilele kikubwa cha mafanikio.
Hizo
ndizo tabia nne ambazo zinawaacha wengi kwenye umaskini, ingawa ule
uwezo wa kupata pesa wanakuwa nao. Fanyia kazi hayo uliyojifunza, chukua
hatua kila siku kuelekea kwenye mafanikio yako.
