Monday, December 14, 2015

Ijuuwe Tuzo Maarufu zaidi Dunia...




Tuzo ya Nobel ni tuzo ya fedha kwa ajili ya mafanikio ya pekee katika fani mbalimbali. Ilianzishwa na Alfred Nobel.

Tangu mwaka wa 1901 imetolewa kwa watu waliofaulu katika fani zifuatazo: Fizikia, Kemia, Tiba (au Fiziolojia), Fasihi na Amani. Tangu mwaka wa 1969, tuzo ya sita imeongezewa kwa Uchumi. Siku hizi Tuzo ya Nobel ni tuzo ya kimataifa mashuhuri kabisa duniani. Wanaotuzwa hupokea hati, medali ya dhahabu na kiasi cha pesa cha takriban € milioni 1,2 (kinategemea mapato ya riba kutokana na mfuko wa fedha iliyotengwa kwa kusudi hii na Alfred Nobel). Maazimio kuhusu tuzo za kila mwaka hutolewa kufuatana na wasia wa Alfred Nobel na kamati zifuatazo:



  • Tuzo ya Nobel ya Fizikia inateuliwa na Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden
  • Tuzo ya Nobel ya Kemia inateuliwa na Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden
  • Tuzo ya Nobel ya Tiba inateuliwa na Karolinska Institutet Stockholm
  • Tuzo ya Nobel ya Fasihi inateuliwa na Taasisi ya Taaluma ya Sweden kwa lugha na fasihi
  • Tuzo ya Nobel ya Amani inateuliwa na kamati ya Nobel ya Norway iliyochaguliwa na Bunge la Norway
  • Tuzo ya Nobel ya Elimu ya Uchumi inateuliwa na Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Sweden
Alfred Nobel (21 Oktoba 1833 – 10 Desemba 1896) alikuwa mhandisi na mwenye viwanda wa nchi ya Sweden. Mwaka wa 1867 aligundua jinsi ya kutengeneza baruti kali.
Pia aliboresha utoneshaji wa mafuta. Akafaulu kiuchumi akawa mtajiri na wakati uleule mwenye wasiwasi kuhusu matumizi ya baruti aliyogundua kwa sababu aliona matumizi mabaya kwa ajili ya silaha.
Katika hati yake ya wasia alianzisha Tuzo ya Nobel kwa ajili ya mafanikio ya kisayansi lakini pia kwa ajili ya amani duniani.
Na kuanzia ilipoanzishwa tuzo ya Nobel watu mbalimbali wametunukiwa tuzo hii km vile Koblo,Alekapanywa,Nelson Mamndela etc.