Monday, August 24, 2015

Sarafu ya Afica Kusini Imepotomoka...

Sarafu ya Afrika Kusini ,Rand, imeporomoka hadi kiwango cha chini zaidi ikilinganishwa na ile ya dola na hivyobasi kusababisha hasara kubwa katika miezi 19 huku kukiwa na wasiwasi kuhusu ukuwaji mdogo wa uchumi wa China.
Sarafu hiyo ilishuka na kubadilishana kwa 14 dhidi ya dola .
Ni sarafu ambayo imeathiriwa vibaya zaidi miongoni mwa masoko 25 yanayoinuka baada ya wawekezaji kuuza mali zao zilizo hatarini zaidi kutokana na wasiwasi wa ukuwaji wa uchumi wa taifa la uchina ambao ni wapili kwa ukubwa duniani.

Thursday, August 13, 2015

Mawe Yenye Uwezo Wakutengeneza Karatasi..

Kikawaida tunajuwa karatasi hutengenezwa kwa Mbao!!
Lakin Ukifika Nchini Taiwani Unaweza Ukastaahabu kuona au kusikia Jinsi ambavyo mawe yana Tengeneza Makaratasi!!

Ijuwe Aina nyingine ya Miwani "Privacy Glasses" na Maajubu yake

Japan National Institute of Informatics imekuja na teknolojia mpya ya miwani inayoitwa “Privacy Glasses”.
Hii ni miwani inayoweza kuuficha uso wako mbele ya camera zozote na pia ni miwani yenye uwezo ya kuficha uso wa mtu mbele ya mashine yoyote.
Ubunifu huu unaiwezesha miwani hiyo kufyonza mwanga wowote unaoipiga miwani hiyo na pia kuwezesha kuuficha uso wa mtu mbele ya camera au computer yoyote ile, kizuri zaidi ni kwamba majaribio yaliofanyika yametoa majibu chanya kwa asilimia 90% ya bidhaa hiyo..