Hifadhi ya Taifa ya GOMBE ni
hifadhi iliyoanzishwa maalumu kwa ajili ya tafiti za
Kisayansi hususani katika kuwalinda na kuwahifadhi
Wanyamapori adimu wa jamii ya Sokwe mtu (chimpanzees) ambao
wapo hatarini kutoweka duniani (Endangered
species).
Hifadhi hii ya Gombe
ilianzishwa rasmi mwaka 1968 mkoani Kigoma katika
mwambao wa ziwa Tanganyika, upande wa mashariki
takribani umbali wa kilomita 24 kwa njia ya usafiri wa maji
ya Ziwa Tanganyika Kaskazini mwa Mji wa Kigoma.
Hifadhi hii
imegawanyishwa katika kanda 4 ambazo ni pamoja na kanda
za fukwe , kanda za ziwa, kanda za maeneo ya mapori, msitu na
utawala wa hifadhi.
 |
Usafiri wa Boti hutumika Zaidi kwa Watu wanao Safiri Kuelekea katika Hifadhi ya Gombe
|

|
Maporomoko ya maji ya Kalambo vile vile hutirirka na kuingia
katika hifadhi za taifa za Gombe
|
 |
Huu ni Ufukwe wa Ziwa Tanganyika katika Hifadhi ya Gombe
|